ARDHI BLOG

TANGAZO KWA WANANCHI WENYE VIWANJA VILIVYOPIMWA LAKINI HAWANA HATIMILKI

 

Serikali imeazimia kuhakikisha kuwa viwanja vyote vilivyopimwa kote nchini vinamilikishwa. Hivyo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapenda kuwatangazia wananchi wote wenye viwanja vilivyopimwa au nyumba zilizojengwa kwenye viwanja vilivyopimwa kuwa wafike katika ofisi za Ardhi za Halmashauri husika ili waweze kuandaliwa hatimilki kwa viwanja hivyo. Ofisi za Kanda za Wizara zitasimamia zoezi hili ili kuhakikisha kuwa kila Halmashauri inaandaa hatimilki kwa viwanja vyote vilivyopimwa nchini. Zoezi hili limelenga kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na milki salama, kuondoa migogoro ya ardhi na kuwawezesha wananchi kutumia ardhi yao kama dhamana ya mikopo kwenye taasisi za fedha.

Timu ya watendaji na wataalam kutoka Wizarani itatembelea Halmashauri mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa wamiliki wa viwanja vyote vilivyopimwa wanapatiwa hatimilki haraka. Wananchi wote wenye tatizo hili wanatakiwa kufika kwenye Ofisi za Ardhi za Halmashauri zao ili kupata maelekezo zaidi juu ya zoezi hili.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

MKAKATI WA UTOZAJI WA FAINI KWA WAMILIKI WA ARDHI WALIOKIUKA MASHARTI YA UENDELEZAJI NA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapenda kutoa mwenendo wa utekelezeji wa mikakati yake ya ukusanyaji wa maduhuli (makusanyo) ya Serikali. Katika mwaka huu wa fedha 2015/2016, mojawapo ya mikakati yake katika kuhakikisha Wizara inafikia lengo la kukusanya Tsh. 70 bilioni ni:
1. Kuwafikisha mahakamani wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi ambao hawatolipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati na;
2. Kuwatambua pamoja na kuwatoza adhabu wamiliki wote wa ardhi nchini waliokiuka masharti ya uendelezaji kwa kubadili matumizi ya maeneo yao bila kibali.
Taarifa na Mwenendo wa Mkakati wa Kutoza Faini kwa Wamiliki Waliokiuka Masharti ya Uendelezaji
Ndani ya mwezi mmoja na nusu (kuanzia mwezi Februari 2016) tumewafikia wamiliki wa ardhi 679 katika maeneo ya Sinza na Kijitonyama. Tumekagua maeneo yao na kufanya uthamini wa maendelezo kwa wale waliokiuka masharti ya matumizi yaliyopangwa. Katika zoezi hili TUMEBAINI UKIUKWAJI WA MASHARTI YA UENDELEZAJI KWA KUBADILI MATUMIZI YALIYOAINISHWA KATIKA MILIKI ZAO Mfano; Mtu aliyemilikishwa ardhi kwa matumizi ya makazi ameibadili bila kibali na kugeuza kuwa maduka kwa ajili ya shughuli za biashara, nyumba za kulala wageni, hostel n.k. hivyo kuikosesha mapato Serikali kwa kutolipa kodi ya ardhi inayostahili na hata kuwa kero kwa wamiliki wengine.
Kutokana na uthamini uliofanyika kwa kipindi kilichotajwa hapo juu, Serikali inatarajia kukusanya jumla ya Tsh. 854,238,791.5 kama faini kutokana na ubadilishaji wa matumizi ya maeneo usiozingatia Sheria za Ardhi. (Hii ikiwa ni Sinza na kijitonyama)
Zoezi linaloendelea kwa sasa ni kusambaza ilani za kuwataka wamiliki hao kueleza ni kwanini wasitozwe faini ndani ya siku 45, ambalo linafanywa na kampuni ya udalali ya YONO. Baada ya siku hizo kukamilika bila ya kuwasilishwa sababu za msingi za kutokulipishwa faini, mmiliki wa eneo lenye mabadiliko ya matumizi atatakiwa kulipa faini hiyo. Hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani na kupokonywa hati milki.
Mwenendo wa Ukusanyaji Kodi ya Pango La Ardhi.
Mpaka kufikia sasa Wizara imekusanya takribani Tsh.60 Bilioni ambayo ni 85% ya lengo la kukusanya bilion 70 zilizopangwa kukusanywa katika mwaka wa fedha 2015/16 unaoishia mwezi Juni mwaka huu. Ni imani yetu kuwa, lengo hilo tutalifikisha kulingana na mikakati madhubuti wizara iliyoiweka.

Mikakati:
1. Wizara kushirikiana na Ofisi zake za kanda, imesambaza timu za maafisa wake ili kuhakikisha Halmashauri na Manispaa zinasambaza hati za madai ya kodi ya pango la ardhi na kuwafikia wadaiwa wote hasa wakubwa ili kuhakikisha fedha za hizo za Serikali zinalipwa kabla hatua za kisheria kuchukuliwa.

2. Maafisa wateule wa kodi ya pango la ardhi tayari wako mikoani kufungua mashauri ili kupata kibali cha mahakama cha kukamata mali kwa wadaiwa sugu au kupokonywa hati milki. Kwa Jiji la Dar es Salaam mashauri yataanza kusikilizwa katika Baraza ya Nyumba na Ardhi la Wilaya ya Kinondoni kuanzia mwezi Mei, 2016 na kisha zoezi litaendelea kwa mikoa na wilaya zote za jiji la DSM.
Kodi ya Ardhi kwa Mashirika na Taasisi za Umma.
Mpaka sasa Wizara inayadai mashirika na Taasisi za Umma si chini ya bilioni 14 kama kodi ya pango la ardhi kwa maeneo mbalimabali wanayomiliki. Mashirika mengi yamekuwa hayalipi kodi ya pango la ardhi kwa kufikiri kwamba hayapaswi kufanya hivyo.
Naomba kuwajulisha kuwa hakuna msamaha wa kodi ya ardhi utakao tolewa kwa shirika lolote hivyo tunaomba malipo husika yafanyike mapema kuepuka adha ya kufikishwa mahakamani pamoja na kushikwa mali za mashirika hayo.
Rai kwa Umma
Kodi ya ardhi inatozwa kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999, chini ya fungu la 33. na tungependa kuweka wazi kuwa kodi hii ni ya pango la ardhi (Land rent) na si kama kodi nyinginezo, yaani ni ‘non taxable revenue’. Rai yetu kwa wananchi waliopata fursa ya kumiliki maeneo yaliyopangwa na kumilikishwa kisheria, tunawaomba walipe kodi ya pango la ardhi kwa wakati kuepuka usumbufu wa kufikishwa mahakamani, kukamatiwa mali ili kufidia kodi hiyo na hata kufutiwa umiliki wa ardhi.
Wizara inawataka wale wote waliokaguliwa, kufanyiwa uthamini na kupata ilani wafike Wizarani katika ofisi za malipo zilizopo jengo la Kodi, kwa wepesi bila ya usumbufu na kupata ufafanuzi. Tunapenda wananchi wafahamu kuwa zoezi hili ni endelevu ili kuepuka tabia iliyozoeleka ya kubadili matumizi bila kuzingatia sheria za mipango miji na hatimaye kuwa kero kwa wananchi wengine. Zoezi hili linatarajiwa kuendelea katika maeneo mengine hapa Dar es Salaam, na mikoani kwa kushirikiana na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Kanda.

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YAENDELEA NA UTATUZI WA MIGOGORO

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabulla akisisitiza jambo alipokutana na wananchi Wilayani Bukoba na kupokea kero zao zinazohusu sekta ya ardhi.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya ziwa Joseph Shewiyo akitoa ufafanuzi juu ya sheria, kanuni na taratibu zinazotumika katika kutoa huduma kwa wananchi kwenye mkutano wa kupokea kero za sekta ya Ardhi Wilayani Bukoba. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabulla na katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Richard Mihayo

Mwananchi aliyefika katika Mkutano akitoa kero yake kwa Mhe. Angelina Mabulla ,Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokutana na Wananchi katika Ukumbi wa St. Francis Manispaa ya Bukoba.

UIMARISHAJI MIPAKA YA KIMATAIFA KATI YA TANZANIA NA UGANDA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda katika mkutano wa pamoja wa wataalamu kutoka nchi zote mbili uliofanyika Bukoba mkoani Kagera.

Baadhi ya wajumbe ambao pia ni wataalamu kutoka Sekta mbalimbali nchini Tanzania, waliohudhuria mkutano wa pamoja wa kuimarisha Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Bukoba – Kagera

Wajumbe kutoka Tanzania na Uganda waliohudhuria mkutano wa pamoja wa watalaamu mbalimbali juu ya uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili katika picha ya pamoja baada ya mkutano

Wataalamu kutoka Tanzania na Uganda wakikagua mawe ya mipaka (Boundary Pillars)

Moja kati ya Jiwe Kubwa linaonyesha mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Uganda

WAZIRI WA ARDHI AKUTANA NA WAMILIKI WA MABENKI NCHINI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kushoto ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA).

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa na Wamiliki wa Mabenki Nchini wakati alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa katika kikao na Wamiliki wa Mabenki Nchini ili kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kulia ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA), kushoto ni David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara-NHC na Mary Makondo Kaimu Kamishna wa Ardhi.

Baadhi ya Wamiliki wa Mabenki Nchini wakiwa katika kikao hicho.

MFUMO FUNGANISHI WA KIELEKTRONIKI KWA AJILI YA USIMAMIZI WA SEKTA YA ARDHI

Mratibu wa Programu ya mfumo funganishi wa kielekroniki kwa ajili ya usimamizi wa sekta ya ardhi (Integrated Land Information System /ILMIS) Barney Laseko akitoa taarifa fupi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo kwa kamati ya ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii – Dar es Salaam.

Baadhi ya vifaa vya upimaji vya kisasa vinavyoendana na mfumo mpya wa upimaji/ Digital equipment, vitakavyotumika sambamba na mfumo wa funganishi wa kielekroniki kwa ajili ya usimamizi wa sekta ya ardhi.

WIZARA YA ARDHI YABORESHA MIFUMO YA UTOAJI WA HUDUMA

Msajili wa Hati Msaidizi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Apollo Laizer akitoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria na kanuni wanapotaka kumiliki Ardhi ili kuepusha migogoro ya Ardhi. Kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathaniel Methew.

 

Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu maboresho katika kuwahudumia wananchi kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja.

 

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathaniel Methew akiwaeleza waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kuboreshwa kwa mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA hali iliyochangia kuongeza tija kupitia kituo cha huduma kwa mteja kilichopo Makao Makuu ya Wizara hiyo na Katika Ofisi zote za Kanda.kushoto ni Msajili wa Hati Msaidizi.

BALOZI WA UJERUMANI NCHINI TANZANIA AMTEMBELEA WAZIRI LUKUVI OFISINI KWAKE

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimfafanulia jambo Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na Mhe. Lukuvi Waziri wa Ardhi (katikati) alipomtembelea ofisi kwake. Kulia ni mjumbe kutoka ubalozi wa Ujerumani Bi. Lena Thiede.

 

 

Mkurugenzi wa bunge la Israel, Bwn. Ronen Plot akitoa zawadi katika ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (Mb), alipofika na ujumbe wake ofisini kwa Waziri, kuzungumza naye kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Israel. Mhe Lukuvi alikuwa akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb).

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelline Mabula (Mb), akisisitiza jambo kwa ujumbe kutoka Benki ya Dunia hivi karibuni, walipofika ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) kufanya mazungumzo mbalimbali katika Sekta ya ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi (Mb), na Naibu wake kushoto kwake; Angelline Mabula (Mb), wakiwa na ujumbe kutoka Benki ya Dunia hivi karibuni, walipofika Wizarani hapo kufanya mazungumzo mbalimbali katika Sekta ya ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akivalishwa vazi la heshima la kimasai kwa kutambua mchango wake katika kumaliza migogoro ya ardhi Wilayani Monduli.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonesha watumishi na viongozi wa Wilaya ya Mbulu ramani ya mpango wa Mji huo.

LUKUVI ATEMBELEA ENEO LA UBOMOAJI WA JENGO LA GHOROFA 16

Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akiangalia maendeleo ya kazi ya ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.

Mafundi wakiendelea na Ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.

BALOZI WA IRELAND NCHINI AKUTANA NA WAZIRI WA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akizungumza na balozi wa Ireland nchini Bi. Fionnuala Gilsenan ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na balozi wa Ireland nchini Bi. Fionnuala Gilsenan (kulia kwake) baada ya kumaliza mazungumzo yao. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya ardhi, Dr. Yamungu Kayandabila na kutoka kulia ni Bi. Maire Mattew kutoka ubalozi wa Ireland nchini.

WAZIRI WA ARDHI AKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa na watendaji wa Wizara ya Ardhi wakati alipokutana nao ili kuboresha utendaji kazi zinazohusu sekta ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

WAZIRI WA ARDHI AGAWA RAMANI KWA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA YA DAR ES SALAAM

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akigawa ramani za mipango miji kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Dar es salaam ili kuwashirikisha wananchi katika kudhibiti uvamizi wa maeneo ya wazi, miundombinu na maeneo ya umma.

WAZIRI WA ARDHI, MHE. WILLIAM LUKUVI AZINDUA PROGRAMU YA KUWEZESHA UMILIKISHAJI ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi akiwa na uwakilishi wa Balozi za Uingereza, Sweden na Denmark wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi akifunia pazia kuzindua Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi akielezea umuhimu wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika kupanga, kupima na kumilikisha Ardhi kwa wote.

 

UZIO ULIOJENGWA KATIKA HOTEL YA GOLDEN TULIP JIJINI DAR ES SALAAM WABOMOLEWA

Serikali imevunja uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam kutokana na umiliki wa eneo hilo kutolewa kwa njia zisizo halali.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongoza Ubomoaji wa maegesho ya magari wa hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam.

Newer posts → Home ← Older posts