ARDHI BLOG

OFISI ZA ARDHI NYANDA ZA JUU KUSINI MAGHARIBI NA HARAKATI ZA ELIMU YA KODI YA PANGO LA ARDHI.

Msafiri Mmassy akigawa vipeperushi, majarida pamoja na kujibu maswali ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa wananchi waliokuwa wakisubiri huduma katika ofisi za Halmashauri za jiji – Mbeya

Wananchi wakisoma vipeperushi vinavyoelezea sheria na taratibu za ulipaji kodi ya pango la Ardhi

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI DKT. ANGELINA MABULA AKAGUA SEKTA YA ARDHI MKOANI KATAVI

Mkazi wa Kata ya Nsemulwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Bibi Maria akieleza tatizo alilo nalo kuhusu huduma za ardhi mbela ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kata ya Nsemulwa mkoani Katavi mara baada ya kusikiliza matatizo yao kuhusu huduma za sekta.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Katavi Bw. George Magembe akitoa maelezo ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya makazi na biashara inayotekelezwa na Shirika mkoani Katavi wilayani Mpanda kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akitoa maelekezo kwa karani wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya –Mpanda, namna bora ya utunzaji kumbukumbu za majalada ya mashauri wakati alipotembelea Baraza hilo ili kufuatilia utendaji kazi wake.

TANZIA

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wa Wizara Bwana Elvis Nyambita Magare, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ramani Idara ya Upimaji na Ramani kilichotokea tarehe 11/11/2016 Nyumbani kwake mtaa Mindu Upanga Jijini Dar es salaam. Ratiba ya kuaga Mwili wa Marehemu ni leo tarehe 14/11/2016 saa 4:00 Asubuhi hadi 7:00 Mchana na Kusafirishwa. Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano tarehe 16/11/2016 Kijiji cha Shirati Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

SERIKALI YAJIPANGA KURASIMISHA MAKAZI HOLELA KATA YA KIMARA NA SARANGA

Diwani Kata ya Kimara Mhe. Pascal Manota akihamasisha wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara kushirikiana na Wataalam wa masuala ya Ardhi ili kuruhu upimaji wa maeneo yao walipofanya mkutano wa uhamasishaji juu ya Urasimishaji wa Makazi holela.

Kaimu Mkurugenzi Urasimishaji Makazi holela Bi. Bertha Mlonda akielezea faida za urasimishaji katika mkutano wa Uhamasishaji kwa wanachi wa Kata ya kimara mtaa wa Mavurunza

Badhi ya wakazi wa Mtaa wa Mavurunza waliohudhuria mkutano wa Uhamasishaji kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela, wakiwasikiliza viongozi wa Serikali za Mitaa (Hawako pichani) pamoja na wataalam kutoka Sekta ya Ardhi walipokuwa wakitoa elimu kwa wakazi hao.

Hamza Khatibu, Mkazi wa Mtaa wa Mavurunza akiuliza swali kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na wataalam wa Sekta ya Ardhi walipokuwa katika mkutano kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela

NAIBU WAZIRI AFANYA ZIARA MKOANI TANGA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akipokea zawadi ya Mbuzi na viroba vya nafaka kutoka kwa mwenyekiti wa wazee wa Kilindi Rajabu Rusewa mara baada ya kufungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Kilindi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati akikagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wilayani Mkinga wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki (mwenye tai) na Meneja NHC Tanga Issaya Mshamba.

Baadhi ya Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Wilayani Mkinga ambazo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameamuru watumishi wa wilaya hiyo waamie ifikapo tarehe 1 Agosti 2016.

 

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (mwenye tai nyekundu) mara baada ya kujadili changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na wananchi wa Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga na kutolea ufumbuzi migogoro ya Ardhi inayowakabili.

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tanga.

MGOGORO WA ARDHI WA KIJIJI CHA MABWEGERE NA VIJIJI JIRANI WILANI KILOSA, MKOANI MOROGORO KUCHUNGUZWA KISHERIA.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akionyesha taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi ya kijiji cha Mabwegere pamoja na vijiji jirani vya Mkoani Morogoro, Wilayani Kilosa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ). Taarifa hiyo iliandaliwa na msuluhishi Bw. Stephen Mashishanga aliyeteuliwa na Waziri wa Ardhi kwa mujibu wa kifungu cha 7 (2) (a) cha sheria ya Ardhi ya vijiji. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya ardhi, Dkt. Yamungu Kayandabila.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Biashara Jacob Mwambegele (Kulia) taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi ya kijiji cha Mabwegere pamoja na vijiji jirani vya Mfulu, Mbigiri, Dumila, Mambwega na Matongolo Wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Taarifa hiyo iliandaliwa na msuluhishi Bw. Stephen Mashishanga aliyeteuliwa na Waziri wa Ardhi kwa mujibu wa kifungu cha 7 (2) (a) cha sheria ya Ardhi ya vijiji. Katikati ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe akitoa ufafanuzi kuhusu mgogoro wa Ardhi wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro alipokutana na Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi na waandishi wa habari ofisini kwake jijini dar es salaam.

MKUTANO MKUU WA TATU WA BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila afungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji.

Baaadhi ya wataalamu wa mipango miji wakiwa katika Mkutano huo

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akikagua maonesho ya Mipangomiji mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji.

WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHINI AUSTRALIA WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA ARDHI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA 2016

Afisa Ardhi, David Malisa akimkaribisha mfanyabiashara Wolkang Pesec kutoka nchini Austarilia alipotembelea banda la Wizara ya Ardhi katika maonesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ndani ya viwanja vya sabasaba 2016.

Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi wakimsikiliza mfanyabiashara Wolkang Pesec kutoka nchini Australia aliyetembelea banda la Wizara katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa 2016 kwa lengo la kujua jinsi Wizara inavyofanya kazi katika kuhudumia wananchi. Kutoka kushoto ni Mwaamkuu Ally, Hellenic Mpetula na Amos Mpugha.

Wageni waliombatana na mfanyabiashara Wolkang Pesec wa nchini Australia wakimsikiliza Mtaalamu kutoka Wizara ya Ardhi aliyekuwa akiwaeleza kazi zinazofanywa na Wizara kwa ujumla

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, MHE. ANGELINA MABULA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA 2016.

Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Angelina Mabula akisikiliza maelezo juu ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zilizobuniwa na Wizara kupitia kwa wataalamu wa Idara ya Nyumba.

Mhe. Angelina Mabula akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea banda la Wizara ya Ardhi katika maonyesho ya sabasaba 2016

Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Angelina Mabula akihojiwa na waandishi wa habari alipotembelea banda la Wizara katika viwanja vya sabasaba 2016

Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Angelina Mabula akiwa na baadhi ya washiriki katika banda la Wizara alipotembelea maonyesho ya sabasaba 2016

Afisa Ardhi, David Malisa akisikiliza wananchi waliofika katika katika banda la Wizara ya Ardhi ili kupata huduma mbalimbali pamoja na elimu ya masuala ya Ardhi

KOREA YASHIRIKIANA NA WIZARA YA ARDHI KUBORESHA UPIMAJI NCHINI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi imepata vifaa vya upimaji (Total Station) na kutegemea kupata mafunzo kuhusu matumizi yake kuanzia tarehe 13 Juni – 16 juni, 2016 kutoka nchini Korea.


Akikaribisha ujumbe wa Wakorea hao Wizarani, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bwn. Justo Lyamuya amesema kuwa vifaa hivyo vya upimaji vitasaidia kuhuisha ramani zilizopitwa na wakati.


Bwn. Lyamuya ameelaza kuwa idadi ya vifaa vya upimaji vitakavyotolewa wakati wa mafunzo, vitakuwa vinne (4), (Total Stations).
Kwa upande wake Munseok Lee, kiongozi wa ujumbe huo, alitoa ufafanuzi kwa vitendo kwa kifupi kuhusu matumizi ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege, isiyokuwa na Rubani (drone) na kuahidi kutoa ufafanuzi wa kina zaidi kwa siku 4 (tarehe 13 – 16 juni), wakati wa mafunzo yatakayofanyika kwa Maafisa waliopo kwenye kada ya Upimaji na Ramani.


Vifaa hivyo vimetolewa na nchi ya Korea kwa nia ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Korea.

Jigez Kim, mtaalam wa upimaji kutoka Korea, akionyesha jinsi ya kufungua kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone) kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mbele ya Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya (haonekani pichani).

Munseok Lee, mtaalam wa upimaji, kiongozi wa ujumbe wa Korea, akionyesha sehemu inapokaa kamera katika kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone) kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya na Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Elizabeth Mrema.

Munseok Lee, mtaalam wa upimaji, kiongozi wa ujumbe wa Korea, akiwa ametoa kamera iliyokuwepo ndani ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone) na kuonyesha kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya na Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Elizabeth Mrema.

Mtaalam, Jigez Kim akionyesha jinsi ya kufungua parashuti inayotumika wakati wa matumizi ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone).

Mtaalam, Jigez Kim akionyesha jinsi ya kufunga parashuti hiyo kuirudisha ndani ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone).

UZINDUZI BARAZA LA ARDHI LUSHOTO

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akikata utepe kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Lushoto

Waziri Lukuvi akihutubia wananchi wa Lushoto mara baada ya kuzindua ofisi mpya za Baraza la Ardhi wilayani Lushoto

RAMANI ZA MIJI NA MITAA

Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi pamoja na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bw. Justo Lyamuya wakiangalia ramani ya Tawala za Mikoa alipokutana na Watendaji wa Wizara ya Ardhi mkoani Dodoma

 

MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA SERIKALI

Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Ardhi wakimsikiliza Mhe. William Lukuvi alipokutana nao kwa lengo la kujua mikakati ya utekelezaji wa ahadi za Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA ARDHI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi akijibu hoja bungeni wakati wa mapitio ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi kwa mwaka wa fedha 2016/2017

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Lukuvi na Naibu wake Mhe.Angeline Mabula , wakifuatilia hoja za wabunge wakati wa mapitio ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angeline Mabula akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Yamungu Kayandabila Nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Ardhi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Mhe. William Lukuvi Waziri wa Ardhi na Naibu Waziri Mhe. Angeline Mabula wakiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara Nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kupitishwa na bunge kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YATOA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU RAMANI SAHIHI YA TANZANIA

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bw. Justo Lyamuya (Katikati) akitoa kauli ya Serikali juu ya Ramani sahihi ya Tanzania inayoonesha mipaka sahihi ya Kimataifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia kwake ni Mpima mkuu wa ardhi Bw. Emmanuel Isangya na kushoto kwake ni Mkurugenzi msaidizi masuala ya Mipaka ya Kimataifa Dkt. James Mtamakaya

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bw. Justo N.Lyamuya (wa kwanza kushoto) akionyesha ramani sahihi ya Tanzania kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ambayo inatambulisha Mipaka ya nchi kwa usahihi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi msaidizi masuala ya ramani Bw. Elvis Magare na katikati ni Mkurugenzi msaidizi masuala ya mipaka ya kimataifa Dkt. James Mtamakaya

UKUSANYAJI WA MAONI YA KUBORESHA SERA YA TAIFA YA ARDHI YA 1995 KANDA YA ZIWA.

 

Mjumbe wa Kamati ya kukusanya maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 Bw. David Malisa akimpa maelekezo jinsi ya kujaza Dodoso la Kukusanya Maoni Mkazi wa Kijiji cha Nyanguge Magu-Mwanza.

Betha Muluu Afisa Ardhi na Maliasili wilaya ya Ngara mkoani Kagera akitoa maoni yake kwenye Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ilipokuwa mkoani Mwanza.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MHE. ANGELINA MABULA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA ARDHI

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Nyumba Upanga jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Nyumba Upanga jijini Dar es salaam

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Nyumba Upanga jijini Dar es salaam

WANANCHI MKOANI TABORA WATAKA SERA MPYA YA ARDHI IMALIZE MIGOGORO YAO

Abdallah Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji.

 

Mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora Shakira Masudi akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora Hanifa Selengu akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.

Mwl. Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.

 

WAKAZI DODOMA WASHIRIKI KUBORESHA SERA MPYA YA ARDHI

Baadhi ya Wadau wa Ardhi wa mkoani Dodoma wakishiriki kupitia na kuiboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ili kukabili changamoto zinazoikabili sekta ya Ardhi ili Kupata Sera Mpya.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Davis Mwamfupe akitoa maoni yake katika kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika mkoani Dodoma.

 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakishiriki kujaza dodoso la maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995.

Home ← Older posts