NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI DKT. ANGELINA MABULA AKAGUA SEKTA YA ARDHI MKOANI KATAVI

Mkazi wa Kata ya Nsemulwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Bibi Maria akieleza tatizo alilo nalo kuhusu huduma za ardhi mbela ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kata ya Nsemulwa mkoani Katavi mara baada ya kusikiliza matatizo yao kuhusu huduma za sekta.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Katavi Bw. George Magembe akitoa maelezo ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya makazi na biashara inayotekelezwa na Shirika mkoani Katavi wilayani Mpanda kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akitoa maelekezo kwa karani wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya –Mpanda, namna bora ya utunzaji kumbukumbu za majalada ya mashauri wakati alipotembelea Baraza hilo ili kufuatilia utendaji kazi wake.