SERIKALI YAJIPANGA KURASIMISHA MAKAZI HOLELA KATA YA KIMARA NA SARANGA

Diwani Kata ya Kimara Mhe. Pascal Manota akihamasisha wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara kushirikiana na Wataalam wa masuala ya Ardhi ili kuruhu upimaji wa maeneo yao walipofanya mkutano wa uhamasishaji juu ya Urasimishaji wa Makazi holela.

Kaimu Mkurugenzi Urasimishaji Makazi holela Bi. Bertha Mlonda akielezea faida za urasimishaji katika mkutano wa Uhamasishaji kwa wanachi wa Kata ya kimara mtaa wa Mavurunza

Badhi ya wakazi wa Mtaa wa Mavurunza waliohudhuria mkutano wa Uhamasishaji kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela, wakiwasikiliza viongozi wa Serikali za Mitaa (Hawako pichani) pamoja na wataalam kutoka Sekta ya Ardhi walipokuwa wakitoa elimu kwa wakazi hao.

Hamza Khatibu, Mkazi wa Mtaa wa Mavurunza akiuliza swali kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na wataalam wa Sekta ya Ardhi walipokuwa katika mkutano kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela