NAIBU WAZIRI AFANYA ZIARA MKOANI TANGA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akipokea zawadi ya Mbuzi na viroba vya nafaka kutoka kwa mwenyekiti wa wazee wa Kilindi Rajabu Rusewa mara baada ya kufungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Kilindi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati akikagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wilayani Mkinga wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki (mwenye tai) na Meneja NHC Tanga Issaya Mshamba.

Baadhi ya Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Wilayani Mkinga ambazo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameamuru watumishi wa wilaya hiyo waamie ifikapo tarehe 1 Agosti 2016.

 

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (mwenye tai nyekundu) mara baada ya kujadili changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na wananchi wa Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga na kutolea ufumbuzi migogoro ya Ardhi inayowakabili.

Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tanga.