MGOGORO WA ARDHI WA KIJIJI CHA MABWEGERE NA VIJIJI JIRANI WILANI KILOSA, MKOANI MOROGORO KUCHUNGUZWA KISHERIA.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akionyesha taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi ya kijiji cha Mabwegere pamoja na vijiji jirani vya Mkoani Morogoro, Wilayani Kilosa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ). Taarifa hiyo iliandaliwa na msuluhishi Bw. Stephen Mashishanga aliyeteuliwa na Waziri wa Ardhi kwa mujibu wa kifungu cha 7 (2) (a) cha sheria ya Ardhi ya vijiji. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya ardhi, Dkt. Yamungu Kayandabila.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Biashara Jacob Mwambegele (Kulia) taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi ya kijiji cha Mabwegere pamoja na vijiji jirani vya Mfulu, Mbigiri, Dumila, Mambwega na Matongolo Wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Taarifa hiyo iliandaliwa na msuluhishi Bw. Stephen Mashishanga aliyeteuliwa na Waziri wa Ardhi kwa mujibu wa kifungu cha 7 (2) (a) cha sheria ya Ardhi ya vijiji. Katikati ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe akitoa ufafanuzi kuhusu mgogoro wa Ardhi wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro alipokutana na Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi na waandishi wa habari ofisini kwake jijini dar es salaam.