WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHINI AUSTRALIA WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA ARDHI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA 2016

Afisa Ardhi, David Malisa akimkaribisha mfanyabiashara Wolkang Pesec kutoka nchini Austarilia alipotembelea banda la Wizara ya Ardhi katika maonesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ndani ya viwanja vya sabasaba 2016.

Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi wakimsikiliza mfanyabiashara Wolkang Pesec kutoka nchini Australia aliyetembelea banda la Wizara katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa 2016 kwa lengo la kujua jinsi Wizara inavyofanya kazi katika kuhudumia wananchi. Kutoka kushoto ni Mwaamkuu Ally, Hellenic Mpetula na Amos Mpugha.

Wageni waliombatana na mfanyabiashara Wolkang Pesec wa nchini Australia wakimsikiliza Mtaalamu kutoka Wizara ya Ardhi aliyekuwa akiwaeleza kazi zinazofanywa na Wizara kwa ujumla