KOREA YASHIRIKIANA NA WIZARA YA ARDHI KUBORESHA UPIMAJI NCHINI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi imepata vifaa vya upimaji (Total Station) na kutegemea kupata mafunzo kuhusu matumizi yake kuanzia tarehe 13 Juni – 16 juni, 2016 kutoka nchini Korea.


Akikaribisha ujumbe wa Wakorea hao Wizarani, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bwn. Justo Lyamuya amesema kuwa vifaa hivyo vya upimaji vitasaidia kuhuisha ramani zilizopitwa na wakati.


Bwn. Lyamuya ameelaza kuwa idadi ya vifaa vya upimaji vitakavyotolewa wakati wa mafunzo, vitakuwa vinne (4), (Total Stations).
Kwa upande wake Munseok Lee, kiongozi wa ujumbe huo, alitoa ufafanuzi kwa vitendo kwa kifupi kuhusu matumizi ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege, isiyokuwa na Rubani (drone) na kuahidi kutoa ufafanuzi wa kina zaidi kwa siku 4 (tarehe 13 – 16 juni), wakati wa mafunzo yatakayofanyika kwa Maafisa waliopo kwenye kada ya Upimaji na Ramani.


Vifaa hivyo vimetolewa na nchi ya Korea kwa nia ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Korea.

Jigez Kim, mtaalam wa upimaji kutoka Korea, akionyesha jinsi ya kufungua kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone) kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mbele ya Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya (haonekani pichani).

Munseok Lee, mtaalam wa upimaji, kiongozi wa ujumbe wa Korea, akionyesha sehemu inapokaa kamera katika kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone) kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya na Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Elizabeth Mrema.

Munseok Lee, mtaalam wa upimaji, kiongozi wa ujumbe wa Korea, akiwa ametoa kamera iliyokuwepo ndani ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone) na kuonyesha kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya na Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Elizabeth Mrema.

Mtaalam, Jigez Kim akionyesha jinsi ya kufungua parashuti inayotumika wakati wa matumizi ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone).

Mtaalam, Jigez Kim akionyesha jinsi ya kufunga parashuti hiyo kuirudisha ndani ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege isiyokuwa na Rubani (drone).