WANANCHI MKOANI TABORA WATAKA SERA MPYA YA ARDHI IMALIZE MIGOGORO YAO

Abdallah Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji.

 

Mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora Shakira Masudi akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora Hanifa Selengu akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.

Mwl. Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.